4 Januari 2026 - 11:25
Ayatullah Khamenei:Mazungumzo na Waandamanaji Halali Yapokelewe na Kusikilizwa, Wachochezi wa Fujo na Ghasia Hawastahili Kusikilizwa Bali Wadhibitiwe

Ayatullah Khamenei amesisitiza utayari wa mazungumzo na waandamanaji halali, huku akionya kuwa wachochezi wa fujo—aliowataja kuwa mamluki wa adui—hawastahili mazungumzo na wanapaswa kuzuiwa kwa sababu ya kueneza kauli mbiu dhidi ya Uislamu, Iran na Jamhuri ya Kiislamu.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Khamenei, amesema: “Tunafanya mazungumzo na waandamanaji halali, lakini hakuna manufaa ya kufanya mazungumzo na watu wanaochochea fujo na ghasia; hawa lazima wazuiliwe na kusimamishwa.”

Amefafanua kuwa watu hao ni wachochezi na mamluki wanaohusishwa na adui, waliosimama nyuma ya wafanyabiashara (waliokuwa wakifanya Maandamano halali), na wakapaza kauli mbiu zao zinazoipinga Uislamu, Iran, na Jamhuri ya Kiislamu.

Kauli hiyo imekuja katika muktadha wa kutofautisha kati ya madai halali ya raia na vitendo vya vurugu vinavyochochewa na mawakala wa nje.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha